Shirika linalowahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema linahofia mamia ya vijana walitekwa nyara mwezi uliopita kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini. Wiki iliyopita shirika hilo lilikadiria vijana 89, baadhi yao wakiwa na umri wa miaka 13, walitekwa nyara na kundi la waasi huko Wau Shilluk, mji unaopatikana katika aneo linalodhibitiwa na serikali katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile. Katika taarifa yake shirika la UNICEF limesema watu wanaoshukiwa kuwateka nyara vijana hao huenda ni wanachama wa kundi la waasi linaloiunga mkono serikali. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia operesheni hiyo kubwa ya utekaji nyara iliyofanyika tarehe 15 na 16 mwezi uliopita wanajeshi waliokuwa na silaha walilizunguka eneo hilo na kuingia nyumba hadi nyumba wakiwachukua vijana waliofikiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 12. Mkuu wa UNICEF Sudan Kusini Jonathan Veitch amesema usajili na utumiaji wa watoto na makundi ya waasi huziharibu familia na jamii.
2 Machi 2015 - 10:15
Msimbo wa Habari: 674257
Shirika linalowahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema linahofia mamia ya vijana walitekwa nyara mwezi uliopita kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini.